UHAKIKI DIWANI YA WASAKATONGE
JINA LA
KITABU;
WASAKATONGE
MWANDISHI; MUHAMMED SEIF KHATIB
MCHAPISHAJI; OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA;
2003
UTANGULIZI
Wasakatonge
ni diwani inayozungumzia hali ngumu ya maisha. Matatizo anayoyataja mshairi ni
magumu kutibika mfano wa saratani, hata hivyo wananchi wakiungana na kupambana
pamoja jamii mpya yenye misingi ya usawa itapatikana. 8/19/2018 Uhakiki wa
Diwani ya Wasakatonge| Kidato cha Tatu na Nne
MAUDHUI
Maudhui
yamejengwa na vipengele vidogo kama;
DHAMIRA
1.
Uongozi mbaya
Jamii
nyingi za kiafrika zinakabiliwa na suala la uongozi mbaya. Wapo viongozi ambao
hawataki kuachia madaraka kama ilivyooneshwa katika shairi la MADIKTETA,
“Mizinga nayo mitutu,
haitoi risasi,
hutoa maraisi,
walio madikteta.”
Ni
ukweli kuwa viongozi madikteta ndio chanzo cha kukosekana kwa maendeleo katika
bala la Afrika.
2.
Matabaka
Migogoro
mingi inaibuka katika jamii kati ya tabaka la wenye nacho na tabaka la
wasionacho katika kugombea mahitaji ya kila siku. Katika shairi la TONGE LA
UGALI, mshairi anasema,
“wanapigana,
waumizana,
wauwana,
kwa tonge la ugali.”
Tunaoneshwa
kuwa tabaka masikini linajaribu kupambana na tabaka tajiri ili liweze kupata
tonge la ugali.
3.
Umasikini
Mshairi
amejadili kwa kina kuhusu tatizo la umasikini, katika shairi la WASAKATONGE,
anaonesha jinsi ambavyo masikini wanavyotokwa jasho kwa sababu ya kufanya kazi
ngumu zenye mishahara ya kijungujiko.
“jua kali na wasakatonge,
wao ni manamba mashambani,
ni wachapakazi viwandani,
lakini bado ni masikini.”
Wasakatonge wanafanya kila jitihada ili waweze
kujinasua kutoka katika umasikini lakini inashindikana na jasho linaendelea
kuwatoka.
4.
Mmomonyoko wa maadili
Dhamira
hii imejadiliwa katika shairi la JIWE SI MCHI. Mshairi anakemea tabia ya
wanawake wanaooana wao wenyewe kana kwamba wanamume wamekwisha. Mshairi
anayalaani mambo haya mapya yanaingia taratibu na kutaka kuharibu tamaduni
zetu.
Ujumbe
1.
Uongozi mbaya ndiyo chanzo cha kukosekana kwa maendeleo katika bara la Afrika.
Ujumbe huu unapatikana katika shairi la MADIKTETA.
2.
Uhusiano wa unyonyaji umesababisha matabaka na masikini ndiye anayeumia. Haya
yamejadiliwa katika shairi la TONGE LA UGALI.
3.
Umasikini ni tatizo sugu katika jamii. WASAKATONGE.
4.
Viongozi wengi hubadilika kama vinyonga hivyo katika uchaguzi, wapigakura wawe
makini. VINYONGA.
Msimamo
Mwandishi
ana msimamo wa kimapinduzi anashauri kuwa, ili kuondoa matatizo yanayojitokeza
katika jamii, lazima jamii ifuate misingi ya usawa na haki kwa wote.
Falsafa
Mwandishi
anaamini kuwa, jamii yenye maendeleo, ni ile inayofuata misingi ya haki na
usawa.
Fani
Muundo
Mwandishi
ametumia miundo hii:
Tathlitha -Ni muundo ambao ubeti mmoja
huwa na mistari mitatu.
Mfano wa mashairi yaliyotumia
muundo huu ni “Nilinde”, “Tutabakia wawili”, “Itoe kauli yako”, “usiku wa kiza”
na “Sikujua”.
Tarbia-Ni muundo unaotumia mistari mine,
nan i muundo unaopendwa kutumiwa na washairi wengi
Mfano wa mashairi yaliyotumia
muundo huu ni “Mahaba”, “Machozi ya
dhiki”, “Mcheza hawi kiwete”, “Sivui maji mafu”
Sabilia- Muundo huu hutumia zaidi ya
mistari sita na kuendeleaka katika beti
Mfano ni mashairi ya “Waso
dhambi”, “Sikuliwa sikuzama”,
“Madikteta”, “Si wewe?”, “Vinyonga”
Mtindo
Mwandishi
ametumia mitindo yote miwili: mtindo wa kimapokeo na mtindo wa kisasa.
Baadhi
ya mashairi ya kisasa ni: “Sikujua”, “Tutabakia wawili” na “Jiwe si mchi”
Baadhi
ya mashairi ya kimapokeo ni: “Mahaba”, “mcheza hawi kiwete” “Sivui maji mafu”
na mengine.
Matumizi
ya Lugha
Vipengele
vya matumizi ya lugha vinajadiliwa.
Tamathali za semi
Tashibiha
“lnanuka kama
ng’onda” – “Kansa”
Sitiari
“Usijigeuze Popo” –
“Itoe kauli yako” “Uchoyo ni sumu” – “Pendo tamu”
Tashihisi
“Inaumwa Afrika” –
“Tiba isotibu” “Radi yenye chereko” – “Afrika” “Pendo lenye tabasamu” – “Pendo
tamu”
Mubaalagha
“Pendo tamu kama
letu duniani hulikuti” – “Pendo tamu”.
Mbinu
nyingine za kisanaa
Takriri
Mfano “nilikesha”- “nilikesha”
“Buzi” – “Buzi lisilochunika”
Matumizi ya semi
Misemo
“mcheza hawi kiwete, ngoma yataka
matao” – “Mcheza hawi kiwete”
Ujenzi wa taswira
“Vinyonga” – “viongozi wasaliti” – “vinyonga”
“Chui na Simba”- “watu wenye mamlaka” – “miamba” “Bundi” – wakoloni wanyonyaji”
– “Bundi” “Vindama”- “nchi zinazoendelea” – “fahali la dunia”. “Fahali la
dunia” – “nchi za ulaya”
migogoro
JibuFutaMbn mnahakiki kidogo
FutaMngekua mnaweka na maswali ya kujipima walimu
JibuFutaMaswal bd mm ni mwanafunz nahitaj ninapomaliza kusoma tukutane nz changamoto changamoto zenyewe ni maswal
JibuFutaMumefanya vizuri ila zidisheni kuhakiki
JibuFuta