1.UANDISHI WA RIPOTI Ripoti ni maelezo kuhusu mtu, kitu au jambo fulani lililotokea. Ni aina ya kumbukumbu ambazo huandikwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Ripoti inaweza kuwa ya uchunguzi wa utafiti kuhusu jambo fulani, inaweza kuwa ya polisi,daktari au ya tume fulani. Namna ya kuandika ripoti Kabla ya kuandika ripoti lazima kuwe na ushahidi unaohusu suala au jambo linaloandikiwa ripoti hiyo. Kwa hiyo, ni lazima mtunzi afanye uchunguzi kwanza. Pia mtunzi anapaswa kufahamu kiwango cha elimu na uwanja wa mtu anayemwandikia ripoti hiyo. Kwa mfano kama ni polisi,daktari,mwanasheria,mfanyabiashara n.k Lugha atakayoitumia mwandishi au mtunzi izingatie muktadha wa matumizi. Lugha itegemee aina ya ripoti. Hatua za uandishi wa ripoti (a) Kichwa cha ripoti Mtunzi aandike kichwa cha ripoti ambacho kinaonesha; kiini cha ripoti- ripoti inahusu nini,tarehe ya tukio au jambo linaloandikiwa ripoti na mahali palipotokea jambo hilo. (b) Utangulizi wa ripoti Katika hatua hii mtunzi hueleza k