UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Uhakiki
wa Ushairi, Tamthiliya na Riwaya
Dhana ya Uhakiki Fafanua vipengele vya
uhakiki Uhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni
juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha
elimu ya sekondari mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo
yanayojitokeza kama vile, dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo
n.k
Dhima
ya Mhakiki na Nafasi ya Mhakiki
Uhakiki ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana
katika kazi za fasihi. Kwa msingi huo uhakiki una dhima zifuatazo:
-Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa
urahisi;Watunzi wa kazi za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na
taswira, hivyo mhakiki anapofanya kazi ya uhakiki anamsaidia msomaji kuelewa
vipengele hivi kwa kuvifafanua kwa lugha rahisi.
-Husaidia ukuaji wa kazi za fasihi;Mhakiki
anapoonesha ubora na udhaifu wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia
watafunguka kifikra na kutunga kazi iliyobora zaidi.
-Uhakiki hukuza uelewa wa mhakiki; Kwa
kuhakiki kazi mbalimbali za fasihi, mhakiki hujiongezea maarifa ya lugha pamoja
na mambo yanayotokea katika jamii.
Nafasi
ya Mhakiki
Mhahiki ana nafasi kubwa katika kazi za
fasihi, Mhakaki ndiye anafafanua kazi ya fasihi ili hadhira iweze kumwelewa
vizuri mtunzi wa kazi hiyo. Kwa hiyo hapa mhakiki anasaidia kurahisisha
mawasiliano kati ya hadhira na mtunzi. Vilevile mtunzi huwaonyesha watunzi
ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya hivyo huwawezesha watunzi kufanya
kazi bora zaidi.
Hatua
za Kufuata wakati wa Kufanya
Uhakiki Vilevile mtunzi huwaonyesha watunzi
ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya hivyo huwawezesha watunzi kufanya
kazi bora zaidi.
-Kwanza ni kuisoma kazi ya fasihi; hapa
mhakiki anatakiwa kuisoma kazi husika ya fasihi kwa kina na kuielewa vizuri.
- Pili ni kuainisha na kuchambua mambo muhimu
yanayojitokeza katika kazi hiyo katika vipengele vya fani na maudhui.
-Tatu
ni kutoa tathimini au kuelezea ubora na udhaifu wa kazi inayohusika.
UHAKIKI WA MASHAIRI
Shairi ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio
maalum wa lugha ya mkato unaowasilisha mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au
mazingira yake na hufuata utaratibu fulani. Mashairi yapo ya aina mbili:
1
Mashairi huru
2
Mashairi ya arudhi
Mashairi ya arudhi
Haya
ni mashairi yanayofuata kanuni za kimapokeo au arudhi za utunzi wa mashairi.
Arudhi/kanuni hizi ni pamoja na:
1
Kugawika kwa shairi katika beti
2 Beti
kuwa na idadi maalum ya mishororo.
3
Mishororo ya ubeti kugawika katika vipande
4
Mishororo kuwa na ulinganifu wa mizani
5
Shairi kuwa na urari wa vina
6
Shairi kuweza kuimbika / kuwa na mahadhi au mapigo.
7
Kuwepo kwa kipokeo katika shairi
8 Kuwa
na mtiririko wa mantiki na mawazo au muwala
9
hairi kuwa na utoshelezo wa beti / kujisimamia kimaana.
Mashairi huru
Pia
hujulikana kama mashairi ya kimapinduzi. Haya ni mashairi yasiozingatia lazima
ya arudhi na hivyo huwa na muundo huru. Sifa zake kuu huweza kuwa:
1
Lugha ya muhtasari
2
Lugha yenye mahadhi
3
Lugha ya kisanii iliyo na mafumbo na taswira
4 Mara
nyingine hugawika katika beti.
5
Mishororo kamilifu (inayojitosheleza) na ile isiyo kamilifu (mishata)
Sifa za Mashairi
Mashairi huwa na sifa maalum
zinazoyatambulisha kama kazi ya kishairi, yawe ya kimapokeo au kimapinduzi.
Sifa hizi ni kama vile:
1
Mashairi hutumia lugha ya mkato / muhtasari
2 Ni
sanaa au kazi iliyobuniwa kwa ufundi
3 Huwa
na mpangilio maalum kuanzia mistari hadi beti.
4
Hutumia lugha teule na msamiati teule uliosheheni tamathali, taswira na
jazanda.
5
Mashairi huwa na sifa ya kuweza kuimbika hivyo shairi ni wimbo na wimbo ni
shairi.
Dhima
ya mashairi
1
Kupasha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya upole na mvuto
2
Kuelimisha na kuzindua jamii.
3
Kuendeleza na kukuza kipawa cha utunzi.
4
Kuhifadhi msamiati wa lugha ya Kiswahili na Sanaa ya fasihi.
5
Kuburudisha hadhira na wasomaji.
6
Kuwasilisha hisia za ndani za mtu na mawazo
Hatua za uhakiki wa mashairi
1 Soma
shairi polepole na kwa makini kupata maana ya jumla.
2 Soma
shairi tena kwa utaratibu ukizingatia maneno na vipande mbalimbali na
kuchunguza maana ya kila mojawapo
3
Pitia maswali yote kwa makini ukitilia maanani aina ya majibu yanayotarajiwa.
4 Soma
shairi tena ukipigia mstari kwa penseli sehemu zinazoelekea kujibu maswali.
5 Toa
majibu kamilifu kulingana na swali kwa lugha ya mtiririko.
Vipengee vya Uchambuzi Wa Mashairi
1
Anwani/kichwa cha shairi – Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno
au sentensi moja. Anwani ni kidokezo muhimu cha kinachozungumziwa katika
shairi. Anwani huweza kuwa ya moja kwa moja, fumbo, kinaya, kibwagizo au sehemu
ya kibwagizo. Ikiwa shairi halina anwani, basi lipewe anwani inayoafikiana na
maudhui au dhamira kwasentensi isiyozidi maneno 6. 2 Maudhui – Haya ni
masuala makuu au mambo muhimu yanayohusu mwanadamu au mazingira yake
yanayozungumziwa katika shairi. Kwa mfano: malezi, siasa, usalama,
unyanyasaji, ufisadi n.k.
2 Maudhui hung’amuliwa kwa wepesi kutokana na kisa
kilichomo katika shairi.
3 Dhamira / shabaha - Ni lengo kuu la mshairi katika
kusanifu utungo wake. Dhamira ya mtunzi huwa ni ujumbe kwa kifupi anaoutambua
msomaji kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi katika
shairi. Mfano: Baada ya kusoma shairi, unaweza kung’amua mtunzi
alitaka kusisitiza kauli kuwa uongozi mbaya haufai, misitu ni
uhai n.k. Dhamira hutokana na mwelekeo wa mawazo ya mshairi au falsafa
yake.
4 Mbinu na tamathali za lugha - Ni mbinu za uandishi na tamathali za
usemi zilizotumiwa na mshairi katika shairi. Mfano:
-Mazda / ziada / zidi - kurefusha
maneno;enda kuwa enenda.
-Inksari / muhtasari - Ni kufupisha
maneno;aliyefika kuwa alofika.
-Utohozi – Mbinu ya kugeuza msamiati /
maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika kana kwamba ni ya
Kiswahili. Mfano: Time - taimu; One – Wani. Mbinu hii vilevile
huitwa ukopaji au uswahilishaji.
-Taarifa Muhimu za Mwandishi wa kila Kitabu
Baini taarifa muhimu za mwandishi wa kila kitabu Mwandishi wa fasihi ni mtu
anaeweza kubuni kazi ya fasihi na kuiweka katika maandishi. Unaposoma kazi za
fasihi ni lazima ujue taarifa muhimu za mwandishi wa kazi hiyo, ambazo ni jina,
kwa sababu kila utakapokua unajibu swali ni lazima utaje jina la mwandishi wa
kitabu.
-
Falsafa na utamaduni kujua
msimamo wake, na
muundo kujua mpangilio wa matukio,
-mtindo kujua upekee wake na matumizi ya
lugha.
Maoni
Chapisha Maoni