Mwandishi ; Theobard Mvungi Wachapishaji ; EP & D.LTD Mwaka : 1995 Maudhui Dhamira 1. Kutetea Haki Mshairi anamshauri kiongozi wa nchi aendelee kuwasha moto dhidi ya watu wote wanaodhulumu haki za wengine. Katika shairi la MWINYI UMEWASHA MOTO ANGALIA USIZIMWE, mshairi anasema, “Tumaini la wanyonge, kwamba ipo serikali, Ile nchi ya mazonge, ya wenye meno makali, Wanyang'anyao matonge, wanyonge hawana hali, Mwinyi ukiwa mkali, ndio raha ya raia.” 2. Demokrasia Mshairi anapinga mfumo wa chama kimoja. Kwake yeye, mfumo huu, unawanyima watu uhuru wa kutoa maoni yao na kukosoa pale mapungufu yanapojitokea. Shairi hili liitwalo TAIFA WAMELIZIKA liliandikwa kipindi ambacho Tanzania ilikuwa katika mfumo wa chama kimoja. Hata hivyo bado lina uhalisia hasa ukizingatia uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyama vya upinzani leo hii. Mshairi anasema, “Mezikwa demokrasi, Chama kimoja ndo' ngao Watu hawana nafasi, kutetea nchi yao Mawazo ya ukakasi, mawaz