Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2018

NADHARIA ZA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI

Nadharia za uhakiki wa kazi za kifasihi 1. Nadharia ya UFEMINISTI   Neno hili linataja jumla ya harakati na itikadi tofautitofauti zinazolenga kufikia usawa wa haki za wanawake katika siasa, uchumi, utamaduni na jamii kote duniani. Wafuasi wa nadharia hii wanashikilia kwamba, pana haja ya kuwa na usawa wa kijinsia licha ya kuwapo kwa tofauti za kimaumbile Hii ni nadharia ambayo haina muhasisi mmoja wala haina msingi mmoja. wanafeministi hutambulishwa kwa wakati na mahali anapotokea.nadharia hii imepata nguvu mwaka 1995. Nadharia hii hudhamiria kuonyesha kwamba uana na uhusiano kati ya mwanaumena mwanamke ni mambo ya kati kabisa katika fasihi. Wahakiki wanaotumia nadharia hii hujikita zaidi katika kutazama jinsi mwanaume alivyo umbwa katika kazi ya kifasihi na kuacha kuitazama kazi inavyosawili maisha yanayo mzunguka mwanadamu. Nadharia hii ya ufeministi imejikita katika msingi mkuu ambao ni kumkomboa mwanamke dhidi ya kani za maisha zinazomdunisha mwanamke katika nyuga zote za mais