UHAKIKI WA MASHAIRI YA CHEKECHEKA
Mwandishi;
Theobard Mvungi
Wachapishaji;
EP & D.LTD
Mwaka:
1995
Maudhui
Dhamira
1. Kutetea Haki
Mshairi anamshauri kiongozi wa nchi aendelee kuwasha
moto dhidi ya watu wote wanaodhulumu haki za wengine. Katika shairi la MWINYI
UMEWASHA MOTO ANGALIA USIZIMWE, mshairi anasema,
“Tumaini
la wanyonge, kwamba ipo serikali,
Ile
nchi ya mazonge, ya wenye meno makali,
Wanyang'anyao
matonge, wanyonge hawana hali,
Mwinyi
ukiwa mkali, ndio raha ya raia.”
2.
Demokrasia
Mshairi
anapinga mfumo wa chama kimoja. Kwake yeye, mfumo huu, unawanyima watu uhuru wa
kutoa maoni yao na kukosoa pale mapungufu yanapojitokea. Shairi hili liitwalo
TAIFA WAMELIZIKA liliandikwa kipindi ambacho Tanzania ilikuwa katika mfumo wa
chama kimoja. Hata hivyo bado lina uhalisia hasa ukizingatia uminywaji wa
demokrasia na uhuru wa vyama vya upinzani leo hii. Mshairi anasema,
“Mezikwa
demokrasi, Chama kimoja ndo' ngao
Watu
hawana nafasi, kutetea nchi yao
Mawazo
ya ukakasi, mawazo ya mtitio…”
3.
Mapenzi
Mshairi
anaeleza jinsi mapenzi yanavyoweza kumtesa mtu hasa pale unayempenda
anaposhindwa kukuelewa. Katika shairi la NJIWA KIUMBE MTINI mshairi anasema,
“Nimejaribu
kuongea, ndege awe mkononi,
Yeye
juu hurukia, namuomba samahani,
Nyimbo
ananiimbia, nyimbo zachoma moyoni,
Basi
mie taabani, njiwa akitabasamu.”
4.
Uhusiano wa Kimataifa
Katika
shairi la INDIRA, mshairi anaomboleza kifo cha mpigania uhuru wa nchi
hiyo-Indira. Shairi hili linaonyesha jinsi tulivyo na ushirikiano na nchi
nyingine. Mshairi anasema,
“Wengi tumesononeka,
Oktoba kututoka,
Umeondoka haraka,
Kwa kweli ulitukuka.”
5.
Ukasuku
Ukasuku
ni kitendo cha kurudiarudia yale yaliyokwisha semwa. Pia, ni kuandika jambo
bila kutafakari sana. Hapa mshairi anawashauri waandishi wasiwe makasuku.
Anasema,
“Kadhalika
tafakari, Mshairi uwe nyati,
Laghai
usiwakiri, wasikura kwa nyati,
Ati
ukweli ni shari, uwapigie magoti,
Kataa
hotuba tupu, Kandamiza la jamii.”
Ujumbe
1. Viongozi watetee haki za raia wao.
2. Waandishi waepuke ukasuku bali waandike mambo
yatakayosaidia ujenzi wa jamii mpya.
3. Vyama vya upinzani vipewe nafasi ili kuleta
changamoto zitakazochochea maendeleo.
4. Tanzani iendelee kushirikiana na nchi nyingine
kwani umoja ni nguvu.
Falsafa
Mwandishi anaamini kuwa, tukiungana pamoja
tutawezesha ujenzi wa jamii mpya.
Msimamo
Mshairi ana msimamo wa kimapinduzi, matatizo
yaliyopo katika jamii, anaamini yataondolewa endapo watu wataamua kuungana
pamoja.
Fani
Matumizi
ya lugha
Tamathali
za semi
i.
Tashibiha
Moyo
kiburi hatari mfanowe kama radi (uk. 13)
ii.
Tashihisi
Moyo
jifunze busara, iwe ndiyo yako taa
iii. Sitiari
Kadhalika
tafakari, mshairi uwe nyati
Ujenzi
wa Taswira
- Taswira Zionekanazo
Kwa
upande huu wa taswira, tuna mifano michache. Angalia shairi la 'Tuambae
Ukasuku' (uk. 3) lilivyojenga taswira zake. Tutatumia beti zifuatazo:
Hakuna
athubutuye, ati nyati kumtuma
Aibebe
niizigoye, au chuchu kumkama
Na
sogi amjaziye, ampandishe kilima
Nyati
si mkubalifu, mfugaji atazikwa.
Kadhalika
tafakari, mshairi uwe nyati
Ati
ukweli ni shari, uwapigie magoti
Mshairi
jihadhari, usishikwe kama funbo
Usiwe
kama kunguru, woga umejaa tumbo (uk. 3)
Katika mistari hiyo iliyodondolewa, tunaweza kuziona
taswira muhimu za kimaumbile zinazojitokeza. Kwanza, tunaiona taswira ama picha
ya nyati mkali ambayo 'mtu' hathubutu kumtuma mtu. Kuwa na ukali kama wa nyati
si jambo la mchezo, ni la hatari. Tunaweza kuuona ukali wa nyati anayekamuliwa
chuchu. Ni jambo la hatari.
Taswira
za Hisi
Taswira
za aina hii si nyingi katika diwani hii, lakini ni muhimu kuzitaja pia. Katika
shairi lake la 'Kuna Nini Huko Ndani' (uk. 4) tunaisikia sauti ya mshairi
ikisema na kugundua harufu za kunukia. Kunukia huku kunaleta athari za hisia
kali zinazosababisha mtu kuwa na tamaa kali zaidi. Mshairi anasema:
Kuna
nini huko ndani, mbona jiko lanukia?
Rihi
yajaa puani, na muda wajiendea
Kisoiva
kitu gani, inbona mate mwalutoa.
Naona
mwajigawia, mwapishi ninawahofu (uk. 4)
Taswira
za Mawazoni
Taswira
nyingine ni za mawazoni tu. Kwa mfanu, mshairi anatuletea shairi lake moja
ambalo anaongea na 'kimoyo' (uk. 12) chake. Anasema kwa mfano:
Wewe
kimoyo sikia, mbona unanipa tabu?
Si
mimi wanionea, kwamba wewe yakusibu
Ni
pole nakuainbia, pole sina matibabu
Kimoyo,
sinilaumu, uwezo umekuwa haba (uk. 12)
Ingawa tunajua kuwa kila mtu ana moyo, lakini mtu
kuzungumza na moyo ni jambo la mawazoni tu. Linaathiri maisha ya mtu kwa
kuzingatia kweli kwamba mtu huyo ana mgogoro na nafsi yake!
Jammin' Jars Casino Tickets - Kansas City - JTM Hub
JibuFutaJ'TUBET 서귀포 출장샵 CASINO in Kansas City 나주 출장샵 tickets and promo codes for upcoming 세종특별자치 출장안마 events. Use 군산 출장안마 jumba casino coupon code: JTUBET. 남원 출장마사지