UCHAMBUZI WA RIWAYA YA MIRATHI YA HATARI
MIRATHI YA HATARI Mwandishi: C.G MUNG'ONG'O Mwaka: 1977 MAUDHUI Dhamira 1. Uchawi na ushirikina Dhamira hii ndiyo inayotawala riwaya. Gusto anarithi kutoka kwa baba yake tunguri, uwezo wa kiwanga pamoja na visasi na vinyongo vya baba yake. Hivyo, maisha yake yanaingizwa katika ulimwengu wa wachawi na mazingaombwe. 2. Mgongano kati ya mila za kale na maendeleo ya kisasa. Gusto anajikuta katika mvutano kati ya kutekeleza matakwa ya marehemu baba yake na kufuata dhamiri yake pamoja na matarajio ya jamii inayotafuta maendeleo ya kisasa. Hii inaonyesha mgongano kati ya imani za jadi za uchawi na fikra za kisasa. 3. Mirathi yenye madhara Mirathi ya Gusto si mali ya kawaida. Anarithi tunguri, madaraka ya kiwanga, visasi na vinyongo vya baba yake. Urithi huu unamletea matatizo, vitimbi, hasara na mikasa ya kutisha; ndiyo maana unaitwa Mirathi ya Hatari. 4. Tamaa ya madaraka Dhamira hii inajitokeza kupitia hamu ya kuwa na uwezo na madaraka ya kiwanga. Uwezo wa uchawi unahusishwa na n...