UCHAMBUZI WA RIWAYA YA MIRATHI YA HATARI

MIRATHI YA HATARI Mwandishi: C.G MUNG'ONG'O Mwaka: 1977 MAUDHUI Dhamira 1. Uchawi na ushirikina Dhamira hii ndiyo inayotawala riwaya. Gusto anarithi kutoka kwa baba yake tunguri, uwezo wa kiwanga pamoja na visasi na vinyongo vya baba yake. Hivyo, maisha yake yanaingizwa katika ulimwengu wa wachawi na mazingaombwe. 2. Mgongano kati ya mila za kale na maendeleo ya kisasa. Gusto anajikuta katika mvutano kati ya kutekeleza matakwa ya marehemu baba yake na kufuata dhamiri yake pamoja na matarajio ya jamii inayotafuta maendeleo ya kisasa. Hii inaonyesha mgongano kati ya imani za jadi za uchawi na fikra za kisasa. 3. Mirathi yenye madhara Mirathi ya Gusto si mali ya kawaida. Anarithi tunguri, madaraka ya kiwanga, visasi na vinyongo vya baba yake. Urithi huu unamletea matatizo, vitimbi, hasara na mikasa ya kutisha; ndiyo maana unaitwa Mirathi ya Hatari. 4. Tamaa ya madaraka Dhamira hii inajitokeza kupitia hamu ya kuwa na uwezo na madaraka ya kiwanga. Uwezo wa uchawi unahusishwa na nguvu ya kumtawala au kumdhuru mwingine, jambo linaloonyesha jinsi tamaa ya madaraka inavyoweza kuwa hatari. 5. Kisasi na vinyongo Gusto anarithi si uwezo wa kiwanga pekee, bali pia visasi na vinyongo vya baba yake. Hivyo, anabeba migogoro na uadui wa zamani ambao haukuanzishwa na yeye mwenyewe. 6. Madhara ya uchawi katika jamii Riwaya inaonyesha uchawi kama jambo linaloweza kuleta hofu, vitisho, mikasa, hasara na migogoro. Mwandishi anawaacha wasomaji wajiulize kama uchawi na uganga vina manufaa kwa jamii au ni “mirathi ya hatari” katika utamaduni. 7. Elimu dhidi ya imani potofu Gusto ni kijana mdogo wa shule, hivyo anawakilisha kizazi kinachopata elimu na kinachoweza kuhoji imani za kale. Hata hivyo, elimu yake inakabiliwa na nguvu za uchawi na mila alizorithi kutoka kwa baba yake. 8. Wajibu wa mtu binafsi na dhamiri Gusto analazimika kufanya uamuzi mgumu: afuate matakwa ya marehemu baba yake au afuate 9. Maendeleo ya jamii Jamii ya Gusto inaonekana kuwa inatafuta maendeleo ya kisasa. Hata hivyo, maendeleo hayo yanakwamishwa na nguvu za uchawi na imani za kale. Kwa hiyo, mwandishi anaonyesha changamoto inayoweza kuikabili jamii inayotaka kuendelea huku bado ikiwa imeshikiliwa na imani potofu. 10. Hofu na vitisho Katika riwaya, Gusto anakabiliwa na vitimbi, hasara na mikasa ya kutisha kutokana na mirathi aliyopata. Hivyo, hofu inatumika kuonyesha madhara ya kuendeleza au kurithi nguvu za uchawi. 11. Nafasi ya mwanamke katika jamii 1. Mwanamke kama mlezi wa familia. Mfano: Nyamidze, ambaye ni mama yake Gusto, anawakilisha nafasi ya mama katika familia. Anahusika katika maisha na malezi ya Gusto, na matatizo yanayompata Gusto pamoja na familia yake yanamgusa moja kwa moja. 2. Mwanamke kama mshiriki wa kutafuta suluhisho la matatizo. Mfano: Nyamidze anapokumbwa na matatizo, anaenda kwa mganga Mama Tumwene kutafuta msaada. Hii inaonyesha mwanamke akishiriki katika kutafuta suluhisho la matatizo yanayoikabili familia. 3. Mwanamke kama mwathirika wa imani za kishirikina. Mfano: Nyamidze, Dina na Nandi wanatajwa miongoni mwa wahusika wa kike wanaopoteza maisha kutokana na madhara ya mirathi ya uchawi na visasi vinavyohusishwa na Gusto. Hivyo, mwanamke anaonyeshwa kuwa mmoja wa waathirika wa imani na vitendo vya kishirikina katika jamii 4. Mwanamke kama mhusika mwenye nafasi katika masuala ya kiroho. Mfano: Mama Tumwene anaonekana kama mganga ambaye watu humwendea wanapokuwa na matatizo. Hii inaonyesha kuwa mwanamke anaweza kuwa na nafasi ya kijamii na kiroho katika jamii ya jadi. 5. Mwanamke kama mhanga wa migogoro ya jamii Mfano: Vifo vya Dina, Nandi na mama yake Gusto vinaonyesha kwamba migogoro ya uchawi, visasi na mirathi haiathiri wanaume pekee, bali pia wanawake na familia nzima. UJUMBE 1.Tamaa ya mali huleta madhara Mwandishi anaonya kuwa tamaa ya kupata mali au urithi inaweza kumwingiza mtu katika matatizo makubwa. Gusto anapokea mirathi yenye madhara kutoka kwa baba yake Kazembe, jambo linalosababisha mikasa na vifo. 2. Uchawi na ushirikina ni hatari kwa jamii Riwaya inaonyesha kuwa imani za uchawi na ushirikina zinaweza kusababisha hofu, vifo na migogoro katika jamii. Matukio ya kisihiri yanayompata Gusto yanaonyesha hatari ya kuendeleza au kuamini nguvu za kichawi. 3. Matendo mabaya yana madhara Mtu anayefanya matendo mabaya hawezi kukwepa madhara yake. Matendo yanayohusiana na uchawi na mirathi hatari huleta madhara kwa wahusika na jamii kwa ujumla. 4. Mirathi inaweza kuwa chanzo cha migogoro Mwandishi anaonyesha kuwa masuala ya urithi yasiposhughulikiwa kwa busara yanaweza kuleta migogoro, uhasama na hata maangamizi katika familia. 5. Jamii inapaswa kuachana na imani potofu Riwaya inatoa tahadhari dhidi ya kutegemea uchawi na ushirikina katika kutatua matatizo ya maisha. Jamii inapaswa kutumia maarifa, busara na njia sahihi katika kukabiliana na changamoto. 6. Kifo ni sehemu ya maisha Kupitia vifo visivyo vya kawaida vinavyotokea katika riwaya, mwandishi anatukumbusha kuwa maisha ya mwanadamu yana mwisho. Hivyo, binadamu anapaswa kuishi kwa busara na kutenda mema. 7. Uovu humrudia mtenda Ujumbe mwingine ni kwamba mtu anayesababisha madhara kwa wengine anaweza hatimaye kuathiriwa na matendo hayo hayo. Hivyo, jamii inahimizwa kuacha uovu na kuchagua mema. 8. Familia inapaswa kuwa na maelewano Migogoro inayohusiana na mirathi inaonyesha umuhimu wa maelewano, uaminifu na haki ndani ya familia. Tamaa na ubinafsi vinaweza kuvunja uhusiano wa kifamilia. MIGOGORO 1. Mgogoro kati ya Gusto na marehemu baba yake, Kazembe Gusto anarithi kutoka kwa baba yake mirathi ya uchawi, pamoja na nguvu, visasi na vinyongo vya baba yake. Hivyo, Gusto analazimika kukabiliana na urithi huo ambao hakuuomba. Gusto anakuwa katika hali ya kulazimika kuchagua kati ya kutekeleza matakwa ya baba yake au kufuata dhamiri yake mwenyewe na matakwa ya jamii inayotafuta maendeleo. 2. Mgogoro wa Gusto na nguvu za uchawi Gusto anakumbana na vitisho, mikasa na madhara yanayotokana na uchawi na uganga aliourithi. Mfano: Mirathi ya uchawi inahusishwa na visa vya kutisha na vifo visivyo vya kawaida katika jamii. 3. Mgogoro kati ya mila za kale na maendeleo ya kisasa Huu ni mgogoro mkubwa katika riwaya. Upande mmoja kuna imani za uchawi, uganga na mila za kale, na upande mwingine kuna elimu, maendeleo na fikra za kisasa. Mfano: Gusto, akiwa kijana mwenye elimu, anapingana na nguvu za urithi wa uchawi wa baba yake huku jamii ikitamani maendeleo ya kisasa. 4. Mgogoro kati ya Gusto na jamii Jamii ina matarajio fulani kuhusu Gusto na urithi alioupata, lakini Gusto ana dhamiri na mtazamo wake binafsi. Gusto anapaswa kuamua kama atafuata matakwa ya marehemu baba yake au kuyatii matakwa ya jamii inayotaka kuondokana na mambo ya kishirikina. 5. Mgogoro wa ndani ya nafsi ya Gusto Gusto anapambana na nafsi yake kwa sababu anakuwa katika hali ya mchanganyiko wa hofu, mashaka na maamuzi magumu. Anasita kati ya kuendeleza urithi wa baba yake wa uchawi na kuachana nao kwa ajili ya maisha yenye maendeleo na fikra za kisasa. 6. Mgogoro kati ya waumini wa uchawi na wapinzani wa uchawi. Gusto anajikuta akipambana na mazingira ya jamii yenye hofu, uchawi, vitisho na imani za kishirikina.Licha ya kuwa na elimu, Gusto anashindwa kujitenga kwa urahisi na mazingira ya kijamii yaliyomzunguka. FALSAFA Kwa ujumla, falsafa ya mwandishi wa Mirathi ya Hatari ni kwamba jamii inapaswa kutumia elimu, busara na fikra za kisasa kupambana na uchawi, ujinga na imani potofu zinazokwamisha maendeleo. Pia mwandishi anasisitiza kuwa mwanadamu ana wajibu wa kuchagua mema na kupinga urithi au mila zinazodhuru maisha ya watu. MSIMAMO/MTAZAMO Kwa ujumla, mwandishi wa Mirathi ya Hatari ana msimamo wa kupinga uchawi, ushirikina, ujinga na mila potofu zinazokwamisha maendeleo ya jamii; na anaunga mkono elimu, mabadiliko, fikra za kisasa na kupambana na uovu. FANI WAHUSIKA 1. Gusto (Mhusika Mkuu) Kijana wa shule / msomi: Ni mhusika mkuu anayejikuta katikati ya mvutano mkubwa baada ya kurithishwa kinguvu mikoba ya uchawi, nguvu za kiwanga, na visasi vya baba yake. Anakabiliwa na mzozo mzito kati ya misingi ya elimu yake ya kisasa na hofu za kishirikina zinazomkabili.Msimamo: Anasimama kupinga urithi huo wa giza ili kulinda dhamiri yake na maendeleo ya jamii yake. 2. Mzee Kazembe (Baba yake Gusto) Chanzo cha mgogoro: Ni mzee mhafidhina na mchawi mkubwa katika kijiji cha Kiterevadzi ambaye kabla ya kifo chake anamwachia mwanae "mirathi ya hatari". Tabia ya kisasi: Anachorwa kama mtu mwenye vinyongo na chuki, anayeamuru visasi viendelezwe hata baada ya kifo chake. 3. Nyamidze (Mama yake Gusto) Mshika mila na mwoga: Ni mke wa Mzee Kazembe. Baada ya kifo cha mumewe, anakwenda kwa mganga wa kienyeji (Mama Tumwene) kuulizia chanzo cha kifo. Mvuta kamba: Licha ya kuwa mhudhuriaji wa kanisani, bado anaamini nguvu za giza na anamshinikiza Gusto kufuata mila ili kuepuka laana ya marehemu baba yake.Hatama yake: Anakuja kuwa mhanga na kufa kutokana na mlolongo wa visasi na mikasa ya kichawi inayozikumba familia hizo. 4. Nandi (Dada yake Gusto) Mhanga wa visasi: Ni mtoto wa kike katika familia ya Mzee Kazembe. Anawakilisha kundi la watu wasio na hatia wanaouawa kutokana na michezo ya siri ya kiwanga na ulipaji visasi ndani ya jamii. 5. Malipula na Mavengi Wachawi wahasimu: Ni wahusika wanaojihusisha na ulimwengu wa giza na uganga wa siri. Wanawakilisha maadui wa ukoo na ushindani hatari wa kiwanga unaomaliza nguvu kazi na uhai wa wanakijiji. 6. Mjomba Kapedzile. Ndugu wa familia: Ni mjomba wake Gusto ambaye naye anatajwa kuingia na kupoteza maisha kwenye mkondo huo hatari wa vifo vya kishirikina na mazingaombwe. MUUNDO Muundo wa riwaya ya Mirathi ya Hatari ni wa mchanganyiko kwa sababu mwandishi ametumia muundo wa moja kwa moja pamoja na mbinu ya urejeshi katika baadhi ya sehemu. Mfano hadithi inaanza Gusto akiwa kijana msomi anayelazimika kuingia kwenye mambo ya kishirikina. Mwandishi anarudi nyuma kueleza maisha ya Mzee Kazembe. Inajumuisha jinsi alivyopata tunguri zake, jinsi alivyojenga uadui na watu wa kijiji chake, na mazingira yaliyosababisha vifo na laana katika ukoo wao. MTINDO Mwandishi ametumia mtindo wa masimulizi ya kinathari unaochanganya mbinu mbalimbali za kifani ili kuendeleza maudhui na kuwajenga wahusika. Miongoni mwa mitindo hiyo ni: Masimulizi – Mwandishi anasimulia matukio na maisha ya wahusika kwa mtiririko wa matukio. Mazungumzo (dayalojia) – Wahusika huzungumza wao kwa wao, jambo linalosaidia kufichua tabia, migogoro na mawazo yao. Monolojia – Baadhi ya wahusika huwasilisha mawazo au hisia zao kwa kujisemeza. Urejeshi (flashback) – Mwandishi hurudi nyuma kueleza matukio yaliyotokea zamani ili kusaidia msomaji kuelewa historia ya wahusika na matukio ya sasa. Matumizi ya lugha 1. Matumizi ya Methali na Misemo. Mwandishi ametumia methali ili kutoa mafunzo na kuonya mafano; "Mchimba kaburi huingia mwenyewe: "Mbio za sakafuni huishia ukingoni." Unaoonyesha jinsi siri za uovu na urithi wa kishirikina unavyofikia kikomo chake. 2. Matumizi ya Nahau Nahau zimetumika kunogesha mazungumzo na kuonyesha hisia nzito za wahusika. mfano "Kutia mchanga kitumbua" Nahau inayomaanisha kuharibu mipango ya mtu; imetumika pale wahusika wanapopingana kuhusu ugawaji wa mali au siri za kifamilia. "Kula njama" Imetumika sana kuelezea vikao vya siri vya ndugu au waganga wanaopanga mikakati ya kudhuru wengine ili wapate urithi. 3. Matumizi ya Taswira (Lugha ya Picha) Mwandishi anatumia maneno yanayotengeneza picha akilini mwa msomaji ili kuleta msisimko na hofu.Taswira ya giza na dhoruba: Maelezo ya usiku wa giza nene, sauti za ndege wa usiku, au upepo mkali yanapotokea wakati wa matambiko au matukio ya kishirikina. Hii inajenga taswira ya uoga na hatari (horror/suspense).Taswira ya damu: Inayowakilisha ukatili, vifo, na kafara zinazotolewa ili kulinda au kupata mirathi. 4. Matumizi ya Lugha ya Kikundi (Sargon / Jargon)Lugha ya Kitatibu/Kiganga: Utumiaji wa maneno kama "ramli", "nyayo", "ndumba", "matambiko", na "fisi" unalenga kuweka msomaji kwenye ulimwengu halisi wa mambo ya giza na uchawi yanayozungumziwa kwenye riwaya. 5. Matumizi ya Chuzano (Sarcasm) na Kejeli. Wahusika wanapotoleana maneno ya dharau kuhusu umaskini au utajiri wa mashaka, jambo linaloonyesha mpasuko mkubwa wa kijamii na kimaadili kati ya wanaowania mali. KUFAULU NA KUFELI KWA MWANDISHU Kufaulu. Mwandishi wa riwaya Mirathi ya Hatari amefaulu katika uandishi wake kwa sababu ameweza kuwasilisha kwa ufasaha masuala mbalimbali yanayoikabili jamii. Amefaulu kuibua dhamira na ujumbe muhimu unaohusu maisha ya watu, familia, mahusiano na matatizo ya kijamii. Aidha, amefaulu kujenga wahusika wenye tabia na sifa mbalimbali ambao wanaakisi watu halisi katika jamii. Mwandishi pia ametumia lugha ya kisanaa pamoja na mbinu mbalimbali za uandishi kama vile mazungumzo, urejeshi, monolojia na matumizi ya tamathali za semi, jambo ambalo limeifanya riwaya iwe na mvuto na iweze kufikisha ujumbe kwa msomaji. Kwa hiyo, kwa ujumla, mwandishi amefaulu kuunganisha maudhui na fani katika kuwasilisha ujumbe wa riwaya. Kufeli. Kwa ujumla, mwandishi wa riwaya Mirathi ya Hatari amefeli kwa kiasi fulani katika baadhi ya vipengele vya uandishi. Baadhi ya matukio yanaweza kuonekana kuwa ya kupita kiasi au kutokuwa na uhalisia wa kutosha, jambo linaloweza kumfanya msomaji ashindwe kuyaamini kikamilifu. Aidha, baadhi ya wahusika hawajaendelezwa kwa kina na baadhi ya matukio au maelezo yanaweza kuwa marefu na kumchosha msomaji. Pia, baadhi ya mbinu za uandishi zinaweza kufanya mtiririko wa matukio kuwa mgumu kueleweka kwa baadhi ya wasomaji. Hivyo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UHAKIKI WA MALENGA WAPYA

UANDISHI WA RIPOTI NA KUMBUKUMBU ZA MIKUTANO

UHAKIKI WA MASHAIRI YA CHEKECHEKA