NADHARIA ZA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI

Nadharia za uhakiki wa kazi za kifasihi
1. Nadharia ya UFEMINISTI
  Neno hili linataja jumla ya harakati na itikadi tofautitofauti zinazolenga kufikia usawa wa haki za wanawake katika siasa, uchumi, utamaduni na jamii kote duniani. Wafuasi wa nadharia hii wanashikilia kwamba, pana haja ya kuwa na usawa wa kijinsia licha ya kuwapo kwa tofauti za kimaumbile
Hii ni nadharia ambayo haina muhasisi mmoja wala haina msingi mmoja. wanafeministi hutambulishwa kwa wakati na mahali anapotokea.nadharia hii imepata nguvu mwaka 1995. Nadharia hii hudhamiria kuonyesha kwamba uana na uhusiano kati ya mwanaumena mwanamke ni mambo ya kati kabisa katika fasihi.
Wahakiki wanaotumia nadharia hii hujikita zaidi katika kutazama jinsi mwanaume alivyo umbwa katika kazi ya kifasihi na kuacha kuitazama kazi inavyosawili maisha yanayo mzunguka mwanadamu. Nadharia hii ya ufeministi imejikita katika msingi mkuu ambao ni kumkomboa mwanamke dhidi ya kani za maisha zinazomdunisha mwanamke katika nyuga zote za maisha.
Nadharia hii imekuzwa na wanazuoni wakuu wawili waliosaidia kukuza uhakiki wa ufeministi ambao ni
i) Marry Ann Weathers
ii) Gloria Steinam

MARRY ANN WEATHER
Anaamini kwaba ukombozi wa kweri wa mwanamke huanza na mwanamke mmoja na ukombozi huo ni ukombozi wa kifikra . Anasisitiza kwamba kama mwanamke hajakomboka mwenyewe kifikra atawezaje kuwakomboa wanawake wenzake ambao bado wako katika dimbwi la kuwa na mtazamo ambao bado unatakiwa nguvu mbadala ya kumuelimisha kifikra.

GLORIA STEINAM
Mwanazuoni huyu yeye anasema kwamba ukombozi wa kweri wa mwanamke unapatikana pale tu ambapo mwanamke ataweza kujitenga kwa dhati na taasisi mbalimbali kama hizi zifuatazo;
    a) Utamaduni
    b) Dini
     c) Ndoa
Anasisitiza kwamba huwezi kupata ukombozi wa kweri ukiwa bado ndani ya ndoa, utamaduni, na dini kwa sababu kila mfumo unautaratibu wake na utaratibu wake na utekelezaji wake ambao humkandamiza mwanamke na kushindwa kuwa na fikra na mawazo yake binafsi.

MIKONDO YA UFEMINISTI
wengine husema wanaume na wanawake wanapaswa kutendewa sawa katika mambo yote. Wanadhani ya hoja la kijadi kuwa wanawake wana kazi ya kutunza nyumba na kuangalia watoto si sawa na wanaume sawa na wanawake wanapaswa kushiriki katika shughuli hizi sawa.
wengine hukubali kuna tofauti muhimu kati ya jinsia lakinitofauti hizi zisiruhusiwe kuwapa wanauma kipaumbele. Kama wanawake wanapendelea kukaa nyumbani na kuangalia watoto ni sawa lakini wasilazimishwe kufanya hivyo na ya kwamba wanapaswa kupata namna ya malipo kwa kazi hii ama sehemu ya mapato ya familia au pia haki za malipo ya pensheni kutoka serikali kwa wakati wa uzee kwa ajili ya miaka walipotumia kwa kazi ya nyumbani.
wengine husema ya kwamba jamii imepokea utaratibu wake kutokana na mapenziy a wanaume hivyo ni lazima kuwa na aina ya mapindizi katika jamii.
kuna wafuasi wa ufeministi wanaoamini ya kwamba hakuna tofauti za maana kati ya jinsia lakini wengine hufundisha kuwa wanawake ni tofauti kabisa na wanaume.

Hivyo basi nadharia hii ioijikita zaidi kutafuta usawa wa kimaisha kati ya mwanamke na mwanamme kuanglia matendo na ugawanaji haki katika jamii kuwa wote wako sawa katika ukwamuaji wa jamii kisiasa, na kiuchumi.

2. Nadharia ya Unegritude
mwasisi mkubwa wa nadharia ya unegritude ni Leopard Sedar Sengoh na wafuasi wake wa mwanzoni ni Leon-Gontran Dames na Aime Cesaire, hawa wote walikuwa na asili ya nchi za Kiafrika zilizokuwa zikitawaliwa na mfaransa.

Aime Cesaire ndiye mwasisi wa kwanza wa hili neno negritude yaani Negro.
mwanzoni hili neno lilianza kama takwa la kizuoni liloluwa likitumiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu vy ufaransa  na baadae likawa ni dai la kisiasa.
kadri siku zilivyokuwa zikienda mbele unegritude ukawa ni takwa la kifasihi kwa kuandika mashairi tofauti toafauti ( waafrika hao) waliokuwa wanatetea idili za kiafrikana hali ya mwafrika mweusi.
Mwasisi wa nadharia hii Leopard Sengoh alioanisha misingi unaotawala Unegritude, lakini aliainisha misingi mikuu minne.

 MISINGI YA NADHARIA YA UNEGRITUDE
1. Kurudisha asili na thamani halisi ya mwafrika na kurekebisha mifumo ya elimu za kiafrika.
2. Ilitumika kupambana na ukoloni, kutetea uhai na uhalali wa mwafrika.
3 Ikapigania utambulisho wa mwafrika mweusi mbele ya mataifa mengine na rangi zingine. hii imedhihirisha katika nyimbo za msanii nguli wa nyimbo za lege hayati marehemu Luck Dube katika wiimbo wake wa Different colour one peole.
$. Kujenga na kutetea mfumo bainifu wa fasihi na utamaduni halisi wa mwafrika. alisisitiza kuwa kazi za kifasihi zimtazame mwafrika.

3. Nadhari ya U- MARX

Maana ya Umarx:
Wamitila,(2006:182) anasema, umarx ni falsafa ya kiyakinifu hasa kwa kuwa pana msisitizo mkubwa kwenye msingi wa hali za kiyakinifu za maisha kama mazingira ya kuishi kuliko mawazo katika maisha ya binadamu (ikimaanisha kwamba mawazo yake hayategemezi kwenye dhana dhahania kama urembo, ukweli au ndoto bali anayategemeza kwenye uhalisia unaoonekana.
Nadharia ya umarx ilianzishwa na Karl Marx mwaka 1818-1863 na Fredrich Engles (1820-1895).Katika nadharia hii Marx amejikita katika historia na miundo ya kijamii kwa kupitia hoja kuu zifuatazo.
Historia ya maisha ya binadamu inaweza kuelezeka katika misingi yakinifu ya kiuchumi ambayo itachunguza njia za uzalishaji mali pamoja na miundo ya kiuchumi na pia huathiri uzalishaji mali na usambazaji wa mali hizo. Hivi vyote kwa pamoja huunda misingi ambapo kwenye misingi hiyo huunda maadili, itikadi, dini na utamaduni.
Hoja nyingine ni kuamini kuwa historia ya binadamu inadhihirisha au kuakisi harakati zinazoendelea katika matabaka ya kiuchumi-jamii. Marx alisema “Historia ya maisha ya binadamu ni ya harakati za kitabaka”.
Harakati za kitabaka katika jamii. Nadharia ya ki-marx inaangalia matabaka katika ngazi mbalimbali kama vile ngazi ya familia, dini na elimu.
Ubepari kama njia ya uzalishaji mali na mara nyingi huharibiwa na tabaka la chini, hivyo ubepari hujitengenezea njia za kujiharibu wenyewe. Kutokana na unyonyaji na ukandamizaji unaoufanya kwa tabaka la chini.
Njia ya kuondokana na ubepari huu jamii lazima ikemee.
Mshikamano uliopo baina ya tabaka tawaliwa. Kwa mujibu wa marx ili kuondokana na mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji, jamii lazima iungane ili kubadilisha mfumo uliopo.
Matamanio ya kitabaka yanaakisi jamii hiyo au itikadi ya jamii iliyopo. Kwa mujibu wa nadharia ya umarx tabaka la chini itikadi yao ni kupambana na tabaka la juu ili kuondokana na unyonyaji na ukandamizaji na tabaka la juu itikadi yao inaonekana kuwa ni halali kulikandamiza tabaka la chini.
Fasihi inayojitokeza inaweza kuyaakisi au kuyadhihirisha mahusiano ya nguvu katika jamii, matamanio na matakwa ya matabaka yaliyopo katika jamii yanaakisiwa katika itikadi iliyopo katika jamii.
Sifa za Uhakiki wa kimarx:
Kuna muelekeo mkubwa wa kuitazama sanaa katika nadharia hii kwa kutilia mkazo mkubwa kwenye dhamira.
Ni mkabala ambao unaingalia fasihi kwa kuhusisha na mazingira yake ya kihisitoria pamoja na shughuli zingine za kibinadamu.
Ni nadharia inayopinga au mtazamo wa kubagua au kutenga fasihi na mazingira yanayoizaa kama ilivyooneshwa kwenye nadharia nyingine kadhaa.
Kwa kuhimiza kuchunguzwa vipengele vya kijamii na kiuchumi uhakiki unaelekea kupanua uwanda wa fasihi.
Udhaifu wa nadharia hii ya Kimarx:
Uhakiki wa Ki-marx unaishia kuidunisha na kuipuuza kazi ambayo ina sifa za kiwango cha juu sana za kiujumi au kisanaa kwa kuwa ni dhaifu kiitikadi licha ya kuwa itikadi sio kaida au kanuni ya sanaa au ubunifu. Hatuwezi kupuza kazi kwa misingi ya kiitikadi tu.
Hivyo huzichunguza sifa mbalimbali za kazi ya kifasihi pale tu zinapoingiliana na miundo ya kihistoria jamii au kiuchumi kwa kufungamana na itikadi yake.
Matokeo ya mtazamo huu wa kuyamulika zaidi masuala ya kidhamira yanaifanya nadharia hii kutoangaza vipengele vingine vidogovidogo ili kutathimini ubunifu au upekee wa kazi inayohusika.
Unaelekea kuchunguza muktadha wa kihisitoria kwa kuelemea mno kwenye vigezo vya kiuchumi.
Jamii ni kielelezo kinachoshikiliwa kama upeo wa kuendelea na kusambaratika kwa mfumo wa kibepari unaoelekea kuwa na elementi za kinjozi.
Namna ya kutumia uhakiki wa Ki-marx katika kazi za kifasihi.
Miaka ya hivi karibuni uhakiki wa kazi za kifasihi umezidi kupanuka katika kuelezea masuala ya kijamii na kisiasa. Hivyo unapotumia uhakiki wa ki-marx katika kazi za kifasihi lengo ni kuonesha tofauti za kijamii, kisiasa, kiuchumi kulingana na maelezo yalivyo katika kitabu. Hii inaonesha itikadi ya kijamii ya mwandishi na kuweka uhusiano kati ya uzoefu wa kijamii wa mwandishi na wa wahusika wake.
Katika kutekeleza itikadi za uhakiki wa ki-marx kuna hatua tano za kufuata ili kuhakiki kazi ya fasihi kwa ufanisi.
Kueleza jinsi wahusika wanavyohusiana: Uhusiano baina ya watu, muingiliano wao utaonesha madaraja na ishara fulani zinazoendana na tofauti za matabaka ya kijamii.
Kutathimini kazi za wahusika:
Uhusika wao umejikita katika mifumo ya kimatabaka ambapo kazi anayofanya mhusika inaashiria moja kwa moja sehemu alipo katika mfumo. Kiwango cha anasa na kiwango cha utendaji kazi navyo vinaonesha sehemu alipo katika mfumo.
Kuonesha jinsi wahusika wanavyotumia muda wao wa mapumziko. Nadharia ya ki-marx inaeleza kuwa mtu anauwezo wa kutumia muda wake wa mapumziko kwa namna ya uzalishaji mali au anavyopenda yeye. Huu muda wa kupumziko huashiria namna mtu anavyoishi na jamii inayomzunguka.
Kutathimini jukumu la serikali,
kuonesha mfumo wake, vyombo vya utekelezaji na jinsi jamii inavyopokea mafanikio yake.
Kurejea waandishi wengine wa ki-marx na kutafiti vipindi ambavyo kazi hiyo ya kifasihi imechapwa na kisha kuhusianisha mawazo yaliyotolewa na kipindi hicho

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UHAKIKI WA MALENGA WAPYA

UHAKIKI WA MASHAIRI YA CHEKECHEKA

JINSI YA KUJIBU MASWALI YA FASIHI